(GMT+08:00) 2010-01-20 16:48:29
Katika mfululizo wa makala kuhusu safari ya mwandishi wetu wa habari, leo tutazungumzia nchi jirani ya Tanzania, kuhusu maisha na siasa za Baba wa Taifa hilo Julius Kambarange Nyerere.
Watu wa kijiji cha Butiama alikozaliwa, wanasema Marehemu Julius Kambarange Nyerere alikuwa ni kiongozi asiyejitakia makuu.
Nyerere alizaliwa tarehe 13 Aprili mwaka 1922. Aliiongoza Tanzania ambaye mwanzoni ilijulikana kama Tanganyika kuanzia mwaka 1961 hadi 1985 alipostaafu.
Tulisafiri hadi kijiji cha Butiama alikozaliwa Nyerere ili kufahamu zaidi maisha yake na vile alivyokuwa karibu na jamii.
Kwanza tuliingia kwenye nyumba aliyoishi na familia yake wakati akiwa mwalimu, ambayo ni ya kawaida na ni sawa na nyumba nyingine kwenye kijiji cha Butiama.
Jack Nyamwaga ni mzeealiyezaliwa kwenye kijiji hiki cha Butiama na alikua pamoja na Nyerere.
Alinielezea jinsi walivyoishi na Nyerere wakati wa ujana wao na hatimaye baada ya kustaafu kama rais.
Nyerere alikuwa mtoto wa Nyerere Burito aliyekuwa Chifu wa Wazanaki, na alijulikana kama Mwalimu kwa kuwa kabla ya kujiunga na siasa alikuwa mwalimu.
Alijiunga na shule ya Msingi mjini Musoma akiwa na umri wa miaka kumi na miwili na baadaye kujiunga na Shule ya serikali ya wavulana ya Tabora mwaka 1937. Alipata udhamini wa masomo na kujiunga na chuo cha Makerere Kampala Uganda, ambapo alihitimu na Shahada ya ualimu.
Baada ya kuhitimu kwenye Chuo cha Makerere alirejea Tanganyika na kuwa mwalimu katika shule ya sekondari ya St. Mary's iliyoko Tabora.
Baadaye mwaka 1949 Nyerere alipata tena udhamini wa masomo na kwenda kusoma katika Chuo cha Edinburgh.
Nyota ya kisiasa ya Nyerere ilianza kung'aa mwaka 1953 alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama kilichokuwa chama cha wafanyikazi. Mwaka 1954 alibadilisha chama hicho cha TAA kuwa chama cha siasa kwa jina la Tanganyika African National Union(TANU).
Mwaka mmoja baadaye TANU ilisajiliwa na kuwa maarufu kote nchini.
Kutokana na kuhusika kwake katika siasa, Nyerere alijiuzulu kazi yake ya ualimu na kujiunga baraza la serikali ya wakoloni mwaka 1958 na kuwa waziri miaka miwili baadaye.
Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wa ndani na Nyerere akawa Waziri mkuu wa Kwanza tarehe 9 Desemba 1961. Mwaka 1962 alichaguliwa kuwa Rais Tanganyika ilipotangaza kuwa Jamuhuri.
Wakati akiwa Rais Nyerere alishirikiana kwa karibu na China, na China iliisaidia Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ukiwemo mradi mkubwa wa Reli ya Tazara.
Mzee Jack Nyamwaga alinielezea baadhi ya miradi mingine ya China Nchini humo. Akisema,
Lakini kijana mwenye umri mdogo Emmanuel Shije hana ufahamu mkubwa kuhusu Julius Nyerere japo alizaliwa kijijini hapa.
Yeye huambiwa tu kuhusu sifa za kiongozi huyo. Anasema,
Mwaka 1978 jeshi la Tanzania lilikabiliana na lile la Uganda wakati huo Uganda iliongozwa na Idi Amin.
Vita hiyo ilitokanana na hatua ya Uganda kutaka kuteka sehemu ya ardhi ya Tanzania katika mkoa wa Kagera lakini hata hivyo haikufanikiwa.
Baada ya kustaafu mwaka 1985 Nyerere aliendelea kuwa mwenyekiti wa chama cha CCM hadi mwaka 1990, wakati Ali Hassan Mwinyi alipochukua hatamu.
Alirejea kijijini alikozaliwa Butiama kuendeleza shughuli za kilimo, lakini alikuwa na ziara nyingi nchi za nje.
Mwaka wa 1996 Nyerere aliongoza juhudi za kusuluhisha mgogoro wa Burundi.
Mwalimu Nyerere alifariki mjini London Uingereza mwaka 1999 kutokana na maradhi ya Saratani ya Damu na Kuzikwa kijijini Butiama.
Tulitembelea kaburi lake kwenye kijiji hiki ambalo liko karibu na jumba la makumbusho ya Nyerere.
Kwenye jumba hili la makumbusho kuna vitu vingi ambavyo ni kumbukumbu ya Nyerere.
Ben Parajo ni mtoa maelezo kwenye jumba hili.
Baadhi ya vitu vilivyoko kwenye makumbusho haya ni nguo aliyovalia siku ya mwisho alipokwenda kwenye matibabu nchini Uingereza.
Aidha kuna tuzo nyingi alizotunukiwa wakati wa uhai wake.
Hadi leo kijiji hiki cha Butiama alikozaliwa Nyerere kinafahamika kote nchini Tanzania.
Licha ya kuwa siku hizi machifu hawana sifa kubwa nchini humo, Chifu wa Wazanaki wa Butiama bado anaheshimiwa.
Japheth Wazagi sasa ndiye chifu wa wazanaki, na anaishi karibu na nyumba aliyokuwa akiishi Nyerere, yeye alituelezea ukubwa wa jamii ya Wazanaki nchini Tanzania, akisema,
Hayati Julius Nyerere anatambuliwa na watanzania wengi kama baba wa Taifa, mkombozi, msomi, mkulima na kiongozi aliyekuwa karibu na wananchi.

No comments:
Post a Comment