Kufuatia matokeo ya awali ya uchaguzi mdogo wa ubunge huko Biharamulo Magharibi yameonesha kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeongoza kupitia kwa mgombea wake wa ubunde Dk. Anthony Gervas Mbassa.
Matokeo hayo yameonesha kuwa, CHADEMA imeongoza dhidi ya chama tawala cha CCM na TLP. CHADEMA inaongoza kwa kupata 50.2%, huku chama tawala cha CCM kikipata 49% na TLP wakiambulia 0.67%.
Hapo jana hadi kufikia saa 3:00 usiku, mgomea huyo wa CHADEMA alikuwa akiongoza kwa kupata kura 14,607 kati ya kura zilizopigwa, huku bwana Oscar Rwegasira mgombea wa ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alikuwa na kura 14,267 na bwana Mpeka Bahangaza mgombea ubunge kupitia chama cha Tanzania Labour Part (TLP) alikuwa na kura 203, matokeo hayo yalikuwa yakijumuisha kata 7 tu kati ya 8 za jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment